**Taarifa zinasema Waasi wa M23 , wakisaidiwa na Rwanda waliteka #Bunyakiri-Centre siku ya Jumapili na kuendelea kusonga mbele kuelekea eneo la Kambale lililopo umbali wa takriban kilomita tano.
**Kulingana na asasi za kiraia za eneo hilo waasi hao wamesonga umbali wa zaidi ya kilomita 60 ndani ya saa 48.,Kusonga mbele kwa waasi kumezua ukosoaji mkali kutoka kwa wadau wa kiraia katika eneo hilo ambao wanalaumu ukosefu wa mikakati , mbinu na mpangilio mzuri kwa upande wa vikosi vya serikali ya Kongo katika kulinda eneo hilo.
**Watu wamekuwa wanajiuliza jeshi la Kongo limealaaniwa nani mpaka kushindwa kupambana na makundi ya waasi kama M-23??

**Hakika ni mambo yanatia aibu kuona nchi kubwa kama Kongo inashindwa kutengeneza jeshi bora Lenye nidhamu na uwezo wa kupambana na makundi ya waasi kama M-23
***Hakika nimeamini nchi ikikosa jeshi bora na imara na idara imara ya kijasusi itachezewa tu ..
