
**Rwanda imempokea Mtuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari Jean Léonard Teganya baada ya Kufukuzwa kutoka Marekani mnamo tarehe 9 Novemba 2026, ili akabiliwe na mashtaka kuhusiana na madai ya kuhusika kwake katika Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994. ***Teganya alikuwa ni mwanafunzi wa zamani wa udaktari na anayedaiwa kuwa mwanachama wa chama cha MRND pamoja na kundi la wanamgambo wa Interahamwe, anatuhumiwa kushiriki katika kuwaua wagonjwa na wakimbizi wa Kitutsi katika hospitali moja mjini Butare, ambapo wahanga wanadaiwa kuuawa na kubakwa.
***Pia anahusishwa na mauaji ya wanafunzi katika hosteli ya chuo kikuu. Kulingana na Mamlaka ya Taifa ya Mashtaka ya Rwanda (NPPA), Teganya alifunguliwa mashtaka mwaka 2014 kwa tuhuma za mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu.
***Bada ya kukimbia Rwanda mwaka 1994, inasemekana kuwa alipitia nchi kadhaa, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, India na cnada kabla ya kuingia Marekani mwaka 2014.
**Akiwa nchini Marekani alitumikia kifungo cha miezi 97 jela kwa kosa la udanganyifu wa masuala ya uhamiaji na kutoa ushahidi wa uongo, baada ya kuficha madai ya kuhusika kwake katika mauaji ya kimbari wakati wa mchakato wa kuomba hifadhi.
**Kwa sasa anashikiliwa na Mamlaka ya Taifa ya Mashtaka ya Rwanda (NPPA) na anatarajiwa kukabiliwa na mchakato wa kisheria kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.
See less
