
##Mwanamke wa Kwanza kufikia cheo Cha Brigedia jenerali
**Anaitwa Zakia Hussein kutoka nchini somalia ambaye alizaliwa Mwaka 1984, mjini Mogadishu, Somalia.Baba yake Hussein Ahmed, alikuwa daktari binafsi wa rais wa wakati huo wa Somalia, Siyad Barre, huku mama yake akifanya kazi kama afisa mwandamizi katika Benki ya Biashara ya Somalia (Somalia Bank of Commerce)
**Familia ya Hussein ilikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia wakati yeye akiwa na umri wa miaka sita na hatimaye ikahamia nchini Sweden
**Alitumia sehemu kubwa ya utoto wake na kupata elimu nchini Sweden kabla ya kuhamia Uingereza akiwa na umri wa miaka 22..
#Mwaka wa 2012, Zakia Hussein alirudi Somalia na kuanza kufanya kazi kama meneja wa programu katika taasisi ya uchambuzi wa sera ya Heritage Institute jijini Mogadishu.
**Mwaka wa 2014, alijiunga na Jeshi la Polisi la Somalia kama mkurugenzi wa polisi ya jamii, na kuwa mwanamke wa kwanza kabisa kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ndani ya jeshi hilo.
**Pia aliwahi kuwa mkuu wa kitengo cha mipango ya sera na kusimamia uandaaji na utekelezaji wa sera ya mageuzi ya idara kijasusi na Usalama nchini somalia
**Zakia Hussein licha ya Kuwa mtumishi wa polisi ni Afisa wa usalama (intelligence officer) ambaye ni wakala wa idara ya kijasusi wa somalia anayefanya kazi kwenye jeshi la polisi somalia.
**Wakati wa utumishi wake katika jeshi la polisi, Hussein alinusurika katika majaribio mawili ya kuuawa kutokana na ubaguzi wa kijinsia uliokita mizizi pamoja na dharau katika taasisi hiyo iliyotawaliwa na wanaume.
**Hata hivyo, aliendelea na juhudi zake bila kukata tamaa, na mwaka wa 2018 alipandishwa cheo na kuwa Brigedia Jenerali huku akiteuliwa kuwa Naibu Kamishna wa Polisi
**Alikuwa ni mwanamke wa kwanza kufikia cheo Cha Brigedia jenerali katika historia ya vyombo vya usalama vya Somalia.
**Mwaka wa 2021, alianzisha kikosi cha kwanza kabisa cha wanawake pekee katika jeshi maalum lenye silaha nchini Somalia, jambo lililozidi kudhihirisha dhamira yake ya kuwawezesha wanawake nchini humo.
**Hussein akiwa Uingereza alisomea uhusiano wa kimataifa na diplomasia katika Chuo Kikuu cha London Metropolitan,alijihusisha na harakati na utetezi, haswa kwa jamii yake ya asili ya Wasomali hapa tayari alikuwa ameanza kazi yake ya ujasusi .
**Akiwa chuo kikuu huko London, Hussein alikuwa mwanachama hai wa Jumuiya ya Kiislamu na hatimaye akawa makamu wa rais wake , akikabiliana na chuki dhidi ya Uislamu wakati ambapo ilikuwa imeenea.
**Pia alijiunga na harakati ya Hanoolaato, shirika la kijamii na kisiasa linaloongozwa na diaspora linalotetea amani na maendeleo nchini Somalia.
**Alijiunga na Harakati ya Kupinga Ukabila na akaandaa kipindi cha mazungumzo ya lugha ya Kisomali kinachoitwa Hooyo Talkshow in Somalia London Radio,zaidi ya hayo, alijiunga na Hanoolaato na kuwa sauti maarufu ndani ya jamii ya Wasomali huko London.
**Tukumbuke Zakia Hussein anaitwa Brigedia Jenerali ndani ya jeshi la polisi kwa sababu muundo wa Jeshi la Polisi nchini Somalia (Somali Police Force) linatumia vyeo vya kijeshi (General ranks) kwa viongozi wake wa juu kabisa,
