
Watu Wengi wanaamini Tupac bado ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika hip-hop. Alizaliwa New York mwaka wa 1971, alichukua jina lake kutoka kwa kiongozi wa waasi wa Amerika Kusini Tupac Amaru II na kutoa albamu yake ya kwanza mwaka wa 1991.
Tupac Shakur alikuwa, na wengi wanaamini bado ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika hip-hop. Alizaliwa New York mwaka wa 1971, alichukua jina lake kutoka kwa kiongozi wa waasi wa Amerika Kusini Tupac Amaru II na kutoa albamu yake ya kwanza mwaka wa 1991.
Imepita takribani miongo mitatu ya mafumbo, nadharia za njama na maswali yasiyo na majibu kuhusu kifo cha mmoja wa wasanii mashuhuri zaidi katika historia ya muziki wa rap, Tupac Shakur.
Tukio la kupigwa risasi kutoka kwenye gari lililokatisha maisha ya Tupac mnamo Septemba 1996 mjini Las Vegas lilibadilisha mkondo wa muziki wa hip hop na kumgeuza kutoka kuwa nyota mkubwa wa rap hadi kuwa alama ya kudumu ya utamaduni wa kisasa.
Kifo chake kilisalia kuwa mojawapo ya mafumbo makubwa zaidi katika ulimwengu wa burudani. Kwa miaka mingi, kulikuwa na nadharia nyingi kuhusu nani aliyehusika na mauaji hayo, lakini hakuna mtu aliyekuwa amekamatwa au kufunguliwa mashtaka hadi mwaka 2023, wakati Duane “Keffe D” Davis, aliyewahi kuwa kiongozi wa genge la mitaani, aliposhtakiwa kuhusiana na mauaji hayo.
Davis, ambaye sasa ana umri wa miaka 63, alipatikana na hatia ya mauaji na mahakama ya Las Vegas mnamo Agosti 31, 2026. Jobo la majaji lilifikia uamuzi huo baada ya kujadiliana kwa chini ya saa tatu, na hivyo kuhitimisha mojawapo za kesi zilizodumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya muziki wa Marekani.
Kesi hiyo ilifufua kumbukumbu za kipindi cha miaka ya 1990 kilichotawaliwa na ushindani mkali kati ya wasanii wa rap wa Pwani ya Mashariki na Pwani ya Magharibi ya Marekani. Pia ilifichua uhusiano wa karibu uliokuwapo kati ya tasnia ya muziki wa rap na magenge ya mitaani ya Bloods and Crips, uhasama ambao uliangaziwa katika nyimbo, vyombo vya habari na matukio ya wakati huo.
Waendesha mashtaka walidai kuwa mauaji hayo yalifanywa kama kulipiza kisasi baada ya Tupac na baadhi ya watu waliokuwa naye kumshambulia Orlando “Baby Lane” Anderson, mpwa wa Davis, saa chache kabla ya shambulio hilo. Ingawa Davis hakushutumiwa kwa kufyatua risasi, mahakama ilikubaliana na hoja ya upande wa mashtaka kwamba alikuwa mmoja wa walioandaa njama ya mauaji hayo.
Hatimaye, karibu miaka 30 baada ya kifo cha Tupac Shakur, hukumu dhidi ya Davis imeleta sura mpya katika simulizi la moja ya mauaji yaliyotikisa zaidi ulimwengu wa muziki na utamaduni maarufu duniani.
Chanzo cha picha,Getty Images
Tupac Shakur alikuwa, na wengi wanaamini bado ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika hip-hop. Alizaliwa New York mwaka wa 1971, alichukua jina lake kutoka kwa kiongozi wa waasi wa Amerika Kusini Tupac Amaru II na kutoa albamu yake ya kwanza mwaka wa 1991.
