By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
LiwalonaliweLiwalonaliwe
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Kijiweni
  • Dating
  • Career
Search
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Reading: Uganda kuwaondoa wanajeshi wake mji wa Lubero Mashariki mwa DRC
Share
Sign In
Notification Show More
Latest News
M23 yateka tena Rurambo na Munanira; majeshi ya Burundi na Kongo yakabiliwa na shinikizo
Za Kitaa/Street Talks
Anaitwa Albert Rudatsimburwa kutoka Rwanada, kijasusi unaweza kumwita Agent of influence .
Za Kitaa/Street Talks
Luteni Jenerali Emmanuel Karenzi:jasusi na afisa usalama kutoka Rwanda
Kijiweni
Kutana na mh; Mollel Hillary diwani wa kata ya sakina,Arusha anayesifika uchapakazi
Za Kitaa/Street Talks
Huyu ndiye Herzon Ernest mkurugenzi wa kampuni ya Heirz Holding Tanzania,Aleta hamasa kwa vijana wengine Tanzania.
Kijiweni
Aa
LiwalonaliweLiwalonaliwe
Aa
Search
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Focused Affairs
    • Dating
    • Career
    • Kijiweni
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Liwalonaliwe > Za Kitaa/Street Talks > Uganda kuwaondoa wanajeshi wake mji wa Lubero Mashariki mwa DRC
Za Kitaa/Street Talks

Uganda kuwaondoa wanajeshi wake mji wa Lubero Mashariki mwa DRC

Baraka Bitariho
Last updated: 2026/11/27 at 12:02 PM
Baraka Bitariho
Share
SHARE
0
SHARES
ShareTweet

Jeshi la Uganda (UPDF) limetangaza kuwa litawaondoa wanajeshi wake katika mji wa Lubero, ulioko katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ndani ya wiki mbili zijazo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Uganda, usalama wa mji huo utakabidhiwa kwa jeshi la Congo (FARDC) baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Uganda.

UPDF imekuwa ikifanya operesheni katika eneo hilo tangu mwezi Januari 2025, katika juhudi za kuwadhibiti wapiganaji wa kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) waliokuwa wakitoroka mashambulizi ya pamoja ya kijeshi katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Kanali Chris Magezi, Kaimu Mkurugenzi wa Habari katika jeshi la UPDF, haikufafanua sababu za uamuzi wa kuwaondoa wanajeshi hao kutoka Lubero.

Aidha hapo jana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilimwita balozi wa Uganda mjini Kinshasa kufafanua machapisho ya mitandao ya kijamii ya mkuu wa jeshi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mwana wa rais wa nchi hiyo.

Katika mfululizo wa machapisho kwenye mtandao wa X, Jenerali Kainerugaba alisema kuna uwezekano wa waasi kuiteka mji wa Walikale, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa DR Congo.

Uganda na DRC zilianzisha operesheni ya pamoja ya kijeshi mwezi Novemba 2021 dhidi ya ADF na makundi mengine yenye silaha katika eneo hilo, kwa lengo la kudhoofisha na kuangamiza uwezo wao wa kuhatarisha usalama wa eneo hilo

Sign Up For Daily Newsletter

Be keep up! Get the latest breaking news delivered straight to your inbox.
[mc4wp_form]
By signing up, you agree to our Terms of Use and acknowledge the data practices in our Privacy Policy. You may unsubscribe at any time.
Baraka Bitariho November 27, 2026
Share this Article
Facebook Twitter Pinterest Whatsapp Whatsapp LinkedIn Copy Link Print
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

LiwalonaliweLiwalonaliwe
Follow US

© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

[mc4wp_form]
Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Register Lost your password?