Mwaka huu Rais Kagame alimteua Luteni Jenerali
Emmanuel Karenzi ambaye ni mzoefu kwenye masuala ya ujasusi ,usalama Kuwa balozi wa Rwanda nchini China
**Luteni Jenerali wa
Emmanuel Karenzi amewahi Kuwa katibu mkuu idara ya kijasusi Rwanda yani.National Intelligence and Security Services (NISS).
**Amewahi Kuwa mkuu idara ya kijasusi Katika jeshi la Rwanda.
**Amewahi Kuwa mkuu mafunzo na operations za kijeshi nchini Rwanda
**Amewahi Kuwa naibu kamanda wa kikosi maalum Cha Umoja wa Afrika kwenda kulinda amani sudani kusini
*Amewahi Kuwa kati ya makamanda kundi la waasi la National Resistance Army (NRA) waliokuwa wanaongozwa Museveni kupambana na serikali ya Uganda wakati huo.
**Amewahi kuwa kati ya wapiganaji wa kundi la Rwanda patriotic front wakiongozwa na Paul Kagame kwenda kupigana na serikali ya Rwanda wakati huo.
**Amewahi Kuwa kati ya wapiganaji kutoka Rwanda walioenda kumuondoa madarakani rais wa Congo Mabutu seseko wakati huo
**Karake amezaliwa na kukulia nchini Uganda ambapo wazazi wake walikuwa ni wakimbizi kutoka Rwanda.
**Ana degree ya biashara kutoka Chuo Kikuu cha Makerere,nchini Uganda.
**Ana Shahada ya Uzamili ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya
**Pia ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza.
**Amewahi kushiriki mafunzo ya usalama na ulinzi kutoka Chuo cha Jeshi la Afrika Kusini.
**Pia amewahi kushiriki mafunzo ya usalama na ulinzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi nchini Kenya.
#####Kukamatwa kwake.
**Karake amewahi kukamatwa tarehe Mwaka 2015 huko London nchini Uingereza kwa hati yakutoka nchini Uhispania.
**Karake alikuwa amefunguliwa mashtaka mwaka wa 2008 pamoja na maafisa wengine 39 wa vyeo vya juu wa Rwanda kwa uhalifu mkubwa wa binadamu unaodaiwa kufanywa kati ya 1990 na 2002
**Karake alishtakiwa kwa uhalifu mwingi, “ikiwa ni pamoja na mauaji mawili ambayo yaligharimu maisha ya raia wa Uhispania Mwaka 1995 na 1997”.
***Mnamo tarehe 10 Agosti 2015, Karenzi aliachiliwa na mahakama ya Uingereza kwasababu “sheria zinazohusika kwenye kesi hiyo hazijumuishi vitendo vya watu wasio raia wa Uingereza au wakaazi nje ya nchi.
