
#Je unajua hili kwenye ujasusi??
**Kwenye ujasusi Afisa wa usalama mwenye cheo kikubwa (case officer )anaweza kumpa kazi informer kuchunguza,Kufatilia jambo fulani,Alafu informer akamtafuta mtu mwingine amsaidie kufanya kazi hiyo kumbe aliyemtafuta ni Afisa wa usalama intelligence officer ila yeye anakuwa hajui kabisa.
**Afisa wa usalama (intelligence officer) aliyetafutwa na informer ambaye anajua ni mtu wa kawaida ataendelea kufanya kazi bila kufichua utambulisho wake.
**Katika ulimwengu wa ujasusi (espionage) na usalama, kitendo hiki kinaweza kuelezewa Katika dhana mbalimbali mfano
1.sub-sourcing / sub-agent recruitment,Hapa ni hatua ya informer anapewa kazi na case officer Kisha yeye bila idhini au Kwa idhini anaamua kumtumia mtu mwingine wa tatu kumsaidia kukukusanya taarifa hizo ambapo mtu huyo mpya anaitwa sub-source au sub agent
**Pia kitendo hiki unaweza kukiita Double Blind / Unwitting Operation (Operesheni ya Kutokujuana) ambapo watu wanaofanya kazi pamoja hawajui utambulisho wa kweli wa mwingine au hawajui kuwa wote wanafanya kazi chini ya mwavuli mm
mfano Informer (Mtoa taarifa hajui kuwa mtu anayemtafuta kumsaidia ni afisa wa usalama (Intelligence Officer),ila Intelligence Officer anaweza kujua au kutojua case officer aliyemtuma informer maana kwenye idara za kijasusi huko Ulaya / Marekani ni ngumu majasusi wote kujuana maana kuna mfumo kiusalama unaoitwa #Compartmentalization mgawanyo wa siri, nitaelezea mfumo huu siku nyingine.
*Pia unaweza kitendo hiki Blue-on-Blue (Kugongana kwa Maafisa wa Upande Mmoja) hili ni neno la kijasusi linalotumika pale maafisa au idara za kijasusi zinapoingiliana kwenye operesheni bila kujua yani #Caseofficer anamtuma informer kuchunguza mtu alafu Informer anaenda kuomba msaada kwa Intelligence Officer mwingine ambaye anakuwa hajui kama ni afisa wa serikali/idara hiyohiyo bila kujua matokeo yake ni kuwa idara moja inatumia rasilimali zake mara mbili kwenye lengo (target) lilelile bila uratibu.
**Pia unaweza kuita kitendo hiki Blown Cover / Operational Compromise (Kufichuka kwa Siri ya Operesheni)
Kwa upande wa informer, kitendo chake cha kwenda kutafuta msaada wa nje (kwa mtu asiyemjua vizuri) kinaitwa Operational Security (OPSEC) Breach (Uvunjaji wa usalama wa operesheni) badala ya kufanya kazi kwa siri kama alivyoelekezwa na case officer wake, anahatarisha siri hiyo kwa kumhusisha mtu wa tatu ambaye kwa bahati mbaya (au nzuri) anakuwa ni afisa wa usalama.
Katika kanuni za ujasusi informer hapaswi kabisa kumweleza mtu yeyote kuhusu uhusiano wake na idara za kijasusi maana kufanya hivyo ni kuweka maisha yake hatari na kuharibu operesheni nzima.
**Pi Kuna hatari sana mtu aliyetafutwa na informer anatoka upande wa adui atageuzwa #double agent kwa Kumlisha taarifa za uongo #disinformation
