
**Huyu ni Jasusi kutoka Urusi aliyekamatwa Marekani
**Anaitwa Anna Vasilyevna Chapman kwa Kirusi: А́нна Васи́льевна Ча́пман;
**Alizaliwa , tarehe 23 Februari 1982) ni raia wa Urusi ambaye zamani alikuwa jasusi, na sasa ni mtu maarufu katika vyombo vya habari na mwanamitindo; alikamatwa nchini Marekani tarehe 27 Juni 2010 kuhusiana na “Illegals Program,” mtandao wa ujasusi wa Urusi. Wakati wa kukamatwa kwake, alishtakiwa kwa kufanya ujasusi kwa niaba ya shirika la ujasusi Urusi, linalojulikana kama *Sluzhba vneshney razvedki* (SVR)
**Hapo awali alikuwa amepata uraia wa Uingereza kupitia ndoa, uraia ambao aliutumia ili kupata haki ya kuishi nchini Marekani.
**Chapman alikiri mashtaka ya kula njama za kufanya ujasusi nchini Marekani .
**Yeye na Warusi wengine walifukuzwa na kurejeshwa Urusi mnamo tarehe 8 Julai 2010, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa kati ya Urusi na Marekani
**Mwaka 2010 baada ya kufahamu kuwa Chapman alitaka kurejea Uingereza, serikali ya Uingereza ilifuta uraia wake wa na kumzuia kuingia nchini humo.
**Tangu arejee Urusi Chapman amefanya kazi katika nyanja mbalimbali, ikiwemo serikalini kama kiongozi wa baraza la vijana, mwanamitindo katika maonyesho ya mitindo ya Kirusi, na kuendesha kipindi cha televisheni.
