
#Kutana na jasusi aliyefariki Katika kifo cha utata ..
**Anaitwa Jenerali Delphin Kahimbi Kasangwe alikuwa afisa wa ngazi ya juu katika Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC).
**Alizaliwa tarehe 15 Januari 1969, huko Kiniezire, katika Wilaya ya Kalehe mkoani Kivu Kusini.
**Delphin Kahimbi alipata mafunzo ya kijeshi, hasa katika nyanja ya mawasiliano ya kijeshi (signals)—utaalamu unaohusisha mawasiliano na uratibu kati ya vikosi vya jeshi.
**Alijiunga na kundi la waasi la Alliance of Democratic Forces for the Liberation of the Congo (AFDL), vuguvugu lililoongozwa na Laurent-Désiré Kabila kumuondoa rais Mabutu ,Pia alishiriki katika kuunda jeshi jipya la Kongo kufuatia kuanguka kwa utawala wa Mobutu mwaka 1997. Baada ya hapo alihudumu katika majukumu ya mawasiliano ya kijeshi kabla ya hatua kwa hatua kushika majukumu ya kiutendaji na kimkakati ndani ya FARDC.
**Kati ya mwaka 2006 na 2009, alihudumu kama naibu kamanda wa Kanda ya 8 ya Kijeshi mjini Goma, Kivu Kaskazini. **Kuanzia mwaka 2009 hadi 2012, alishiriki katika majukumu ya operesheni za kijeshi zilizojulikana kama Kimya II na Amani Leo zilizofanyika mashariki mwa DRC, hasa mkoani Kivu Kusini.
**Mwaka 2011, aliteuliwa kuwa naibu kamanda wa Kanda ya 10 ya Kijeshi mkoani Kivu Kusini, kabla ya kuhudumu kama naibu kamanda anayesimamia operesheni na ujasusi katika Kanda ya 34 ya Kijeshi mkoani Kivu Kaskazini.
*Mnamo mwaka wa 2014, pia alishikilia majukumu katika mchakato wa kuondoa silaha, kuvunja makundi ya wapiganaji, na kuwarejesha katika jamii (DDR).
**Aidha alishiriki kuongoza ujumbe wa kijeshi wa serikali ya Kongo wakati wa mazungumzo ya Kampala na kundi la M23.
**Alifikia ngazi ya juu Katika jeshi la Kongo alipoteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa mkuu wa Jeshi (Deputy Chief of General Staff) wa FARDC huko akisimamia kitengo cha ujasusi wa kijeshi nafasi aliyoishikilia kwa miaka kadhaa. **Katika nafasi hiyo, alichukua jukumu muhimu katika mfumo wa ujasusi wa kijeshi na usalama wa DRC. **Mnamo Desemba 2016, Umoja wa Ulaya ulimwekea vikwazo kutokana na madai ya kuhusika kwake katika ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa kisiasa nchini DRC,Pia alikuwa miongoni mwa maafisa wa usalama waliolengwa na vikwazo vya kimataifa
** Mnamo Februari 2020, alizuiliwa na Kurugenzi mKuu wa Uhamiaji wa konfgo wakati akijiandaa kusafiri kwenda Afrika Kusini na baadae alisimamishwa kazi. **Alifariki dunia tarehe 28 Februari 2020, jijini Kinshasa, katika mazingira yaliyoibua maswali mengi.
**Meja Jenerali Delphin Kahimbi alizikwa tarehe 6 Desemba 2020, huko Kiniezire—kijiji chake alichozaliwa katika Wilaya ya Kalehe, Kivu Kusini.
**Kifo chake lilikuwa cha utata mkubwa sana .![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
**Kipindi anafariki ndio kulikuwa na mgogoro mkubwa kati Joseph kabila na rais
Felix tshisekedi ambapo rais Felix
Tshisekedi alikuwa anafukuza washirika wa Joseph kabila kutoka serikalini,inadawa ni
Joseph kabila alimwaachia rais
Felix tshisekedi Kwa makubaliano maalum lakini hayo makubaliano yalivunjwa na Felix Tshisekedi
**Baada ya
Felix tshisekedi kuvunja makubaliano na Joseph ambaye alikuwa nguvu na ushawishi Katika vyombo usalama kongo rais felix tshisekedi alikimbilia kufanya urafiki na rais kagame ambapo walikuwa marafiki kubwa lakini kwasasa ni maadui![]()
![]()
![]()
**Baada ya Felix kuvunja urafiki na rais Kagame ndio tukaona kundi la M-23 linarudi Kwa nguvu Kongo
**Pia baada ya Felix tshisekedi kuvunja urafiki na Joseph Kabila ndio tumeona kundi jipya la waasi la AFC linaloongozwa na mzee Nanga wakiingia kwenye vita na serikali ya Kongo , Tukumbuke mzee Nanga ndiye alikuwa mwenyeti wa tume ya Uchaguzi wakati Felix Tshisekedi akitangazea Kuwa rais wa Kongo.
**Kwasasa AFC na M-23 wameungana kupambana na serikali ya Felix Tshisekedi
