ngo
**Komandoo mzalendo aliyeuawa kutokana na kupenda nchi ya Congo
#Anaitwa komandoo Mamadou Mustafa Ndala ambaye alizaliwa 1978 ambaye alifariki mwaka 2014 akiwa na umri miaka 35 tu
#Alikuwa komandoo wa kikosi cha 42 cha Commando Units Rapid Reaction FARDC, ambacho kiliundwa na Ubelgiji, Angola,
Marekani na Uchina.
#Ndala alijiunga na jeshi mwaka 1997 ambapo Mwaka 2011, alipandishwa cheo na kuwa kanali ambapo aliongoza Kikosi cha 42 cha Makomando wa Kitengo cha Rapid Reaction.
#Ndala alisifika na kupendwa na wakazi wa Goma kutokana na uwezo wake kupigania taifa la Congo kwa moyo Moja
#Mwaka 2013, aliongoza mashambulizi makali dhidi ya wapiganaji wa M23 waliouzingira mji wa Goma na kupata ushindi mkubwa.
#Ushindi Ndala dhidi ya M23 uliwafanya watu wa Goma kuondoa mashaka waliokuwa nao kwa jeshi la Congo maana wananchi wa Goma walikuwa wakifanya ghasia za kulalami jeshi lao kutokana kutochukua hatua Kali dhidi ya M23 mfano ni Novemba 2012 wakati M23 walipouteka mji wa Goma,
#Kabla ya M23 kuuteka mji wa Goma Miezi mitatu kabla, katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Ubelgiji Colette Braeckman, Jenerali wa Rwanda ,jasusi mbobezi James Kabarebe alidai kwamba jeshi la Kongo halikuwa na uwezo hata wa kuua panya.
#Wakongo wakiwa katika,huzuni,unyonge na mchanganyiko wa chuki Walistaajabu kuona Komandoo Ndala akiongoza mapambano dhidi M23 mpaka kufikia hatua ya kuonyesha miili ya maadui zao ambapo M23 walipata hasara kubwa.
#Alipata umaarufu kwa ushindi mkubwa dhidi ya wapiganaji M23 mwaka 2013 ..
#Alifariki mwaka 2014 baada ya kuchomwa akiwa kwenye gari lake akiwa na pamoja na wawili baada ya kutokea shambulio la kuvizia, waasi wa Uganda wa ADF ndio walifanya shambulio .
#Katika kuthibitisha usaliti ndani ya jeshi la Congo Wanajeshi wawili wa Jeshi la Congo walipatikana na hatia ya kuajiri waasi wa ADF kutekeleza mauaji ya komando Ndala kwa dola 20,000
