
#Huyu ndiye kiongozi wa upinzani maarufu mwenye nguvu nchini Burundi .
**Anaitwa Agathon Rwasa ambaye alizaliwa Mwaka 1964) ambaye ni mwanasiasa wa upinzani nchini Burundi na pia kiongozi wa zamani wa kundi la waasi la pour la Libération Nationale, FNL).
**Alikuwa kiongozi wa wanamgambo wa Kihutu wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Burundi.
**Rwasa alizaliwa na wazazi wa Kihutu mwaka 1964 huko Ngozi (Kaskazini) mwa Burundi ambapo ni mtoto wa saba katika familia ya watoto 14.
**Alisoma elimu ya msingi na sekondari katika mkoa wa ngozi.
**Akiwa na umri wa miaka 20, aliteuliwa kuwa mkuu wa chama cha wasomi vijana nchini Burundi
**Baada ya kuhitimu masomo yake ya Chuo Kikuu cha Burundi, alitafutwa na serikali kama wasomi kutokana Kuwa na uwezo mkubwa kiakili.
**Wakati wa vita vya wenyewe kwaa wenyewe Burundi anatuhumiwa kuhusika na mauaji huko ya Gatumba-burundi ambapo vifo ya Watutsi 166 walio wachache nchini Burundii vilitokea.
**Baada ya miaka 20 akiwa msituni, alirudi nyumbani mwaka 2008.
**Mwaka 2006 kupitia kundi lake la waasi (FNL) ilitia saini mkataba wa amani na serikali serikali ya burundi.
**Mwaka 2010, Rwasa alijificha, akidai anakabiliwa na kukamatwa na serikali kwa madai ya kuyumbisha usalama wa nchi kufuatia uchaguzi wa wilaya uliofanyika nchini Burundi.
**Mwaka 2015, alichaguliwa kama naibu spika wa Bunge la Burundi.
**Mwaka 2024 aliondolewa kwenye uongozi wa chama chake,kuliandaliwa mkutano wa chama chake Cha
National Congress for Freedom ambapo baadhi ya viongozi wa Chama hicho wakatangaza kumuondoa Agathon Rwasa kwenye uongozi ambapo serikali ya Burundi ilitangaza kukubali maamuzi ya Kumuondoa Agatho Rwanda kwenye Chama Chake
**Agatho Rwanda alidai mkutano huyo ambao ulimuondoa kwenye chama Chake uliandaliwa na serikali ya Burubdi ,Pia akasema wale viongozi Walitangaza kumuondoa ndani ya Chama Chake walitumiwa na serikali ya Burundi ..
**kutokana na mgogoro kuibuka kwenye Chama cha Agatho Rwanda serikali ya Burubdi ilitangaza kusimamishwa shughuli zote za chama cha Agatho Rwanda
**Agathon Rwasa amekuwa akitoa ushindani mkubwa kwa Chama tawala nchini Burundii kwenye chaguzi mbalimbali.
**Mwaka 2015 mke wa Agathon Rwasa aliponea kuuawa kwa kushambuliwa na risasi…
