

Chama cha PASTEF kimetangaza kuwa Bassirou Diomaye Faye amepoteza sifa za kuwa mwanachama wa PASTEF moja kwa moja kwa sababu amejiunga na chama kingine cha kisiasa kiitwacho Kiraay. Hatua hii inawahusu pia watu wengine 32, akiwemo mawaziri sita waliokuwa wa PASTEF ambao waliamua kubaki serikalini baada ya Ousmane Sonko kuondolewa kwenye nafasi ya Waziri Mkuu mnamo Mei 2026.
Chama hicho kinahalalisha hatua hii, iliyotolewa hadharani siku ya Jumanne, Novemba 17, kwa kusema kwamba mkuu wa nchi amechagua kujiunga na chama kingine cha siasa, yaani Kiraay, ambacho yeye mwenyewe alikianzisha mwezi Julai mwaka huu. Uamuzi huu unahalalisha zaidi mgawanyiko kati ya Bassirou Diomaye Faye na Waziri Mkuu wake wa zamani, Ousmane Sonko, ambaye sasa ni Spika wa Bunge la taifa na kiongozi wa PASTEF.
Bassirou Diomaye Faye si mwanachama tena wa PASTEF, chama kilichompandisha cheo cha urais wa Senegal mwaka wa 2024. Hatua hii ilitangazwa rasmi Jumanne, Novemba 17, baada ya mkutano wa baraza la kitaifa la chama hicho chenye wingi wa viti bungeni, ikiweka rasmi mwisho wa uhusiano wa kisiasa kati ya Rais Faye na chama chake cha zamani kufuatia kuunda kwake chama kipya kiitwacho Kiraay.
Hii si hatua ya kumfukuza kutoka katika chama ambacho Bassirou Diomaye Faye anatokea, anabainisha kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa PASTEF, bali ni ‘kupoteza uanachama wa PASTEF kutokana na ukweli kwamba aliamua kujiunga na chama kingine cha kisiasa — yaani chama cha Kiraay ambacho yeye mwenyewe alikiasisi tarehe 25 Julai mwaka huu.”
Taarifa ya chama inaonyesha zaidi kwamba uamuzi huu ulifanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 6 cha sheria za chama na kwamba unawahusu watu wengine 31, wakiwemo mawaziri sita kutoka PASTEF waliochagua kubaki serikalini walioteuliwa baada ya Ousmane Sonko kufukuzwa kutoka wadhifa wake kama Waziri Mkuu mwezi Mei mwaka hu.
“Kisiasa, mgawanyiko umekamilika”
Uamuzi huu unazidi kuimarisha na kuonyesha wazi mgawanyiko wa kisiasa uliopo baina ya Rais Bassirou Diomaye Faye na kiongozi wa PASTEF, Ousmane Sonko.
Ousmane Sonko amethibitisha kuwa kumekuwa na utengano wa kisiasa kati yake na rais Bassirou Diomaye Faye, akifichua kuwa hawajawasiliana tena ama kwa simu au ana kwa ana tangu mwezi Juni mwaka huu.
Haya yanajiri huku kukiwa na wito mbalimbali wa kuitisha mazungumzo kati yao, ingawa afisa mmoja wa chama cha PASTEF amebainisha kuwa hakuna mkutano wowote unaopangwa kwa sasa. Hivi karibuni, chama hicho kilirasimisha kuondoka kwa Bassirou Diomaye Faye kwenye orodha yake ya wanachama baada ya kuanzisha chama chake kipya kiitwacho Kiraay.
