*Anaitwa Kanali Tom Byabagamba
aliyekuwa Kamanda mkuu wa kikosi cha kumlinda Rais wa Kagame.
*Kanali Tom Byabagamba alikuwa ni kati ya wapiganaji wa kundi la Rwanda Patriotic Front wakati huo wakipigana na serikali ya Rwanda
**Alifariki akiwa gerezani baada ya kuzuiliwa kwa takriban miaka ,12
**Azaliwa nchini Uganda ambapo aliwahi Kuwa mlinzi wa kibinafsi wa Kagame kipindi hicho akiiongoza kundi la Rwanda Patriotic Front kupambana na serikali ya Rwanda .
**Baada ya rais Kagame kuingia madarakani aliongoza kikosi maalum cha kumlinda rais wa Kagame kuanzia mwiaka 2002 hadi 2010,
*Alipoondolewa kwenye kikosi na alipewa amri ya kuripoti makao makuu ya jeshi kwa ajili kupewa majukumu mengine, Baadaye alitumwa katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini.
**Aliporejea Rwanda mnamo Agosti 2014 alikamatwa kwahiyo alikuwa amekaa kizuizini kwa takriban miaka 12.
**Kanali Byabagamba alifunguliwa mashitaka pamoja na shemeji yake, Brigedia Jenerali mstaafu Frank Rusagara, ambaye alifariki mapema mwaka 2025
**Mnamo Machi 2016, Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Rwanda ilimtia hatiani Byabagamba kwa makosa yakiwemo kuchochea uasi, kuchafua sifa ya serikali, kuficha ushahidi na kudharau bendera ya taifa.
**Alihukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na kuvuliwa cheo chake cha kijeshi na medali. Shtaka hilo la dharau lilitokana na madai kwamba alishindwa kuonyesha heshima ipasavyo kwa bendera ya Rwanda alipokuwa akihudumu na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini. **Mnamo Desemba 2019, Mahakama ya Rufaa ilithibitisha hukumu yake lakini ikapunguza adhabu hadi miaka 15, **
Huyu ndiye kanali Tom Byabagamba mlinzi wa rais Kagame aliyefariki akiwa jela
Leave a comment
Leave a comment
