By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
LiwalonaliweLiwalonaliwe
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Kijiweni
  • Dating
  • Career
Search
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Reading: DR Congo yataka maelezo kuhusu vitisho vya jenerali Muhoozi wa Uganda
Share
Sign In
Notification Show More
Latest News
Huyu ndiye Avila Chaula mwanamke mpambanaji na mbunifu anayefanya vizuri kwenye urembo.
Za Kitaa/Street Talks
Iran: Mwimbaji Parastoo Ahmadi amechapwa viboko 74 kwa kuimba bila kuvaa hijabu
Za Kitaa/Street Talks
Nathalie Kienga kachero anayesimamia usalama na ulinzi katika ofisi ya rais nchini Kongo
Za Kitaa/Street Talks
Anaitwa Gina Cheri Walker Haspel Afisa usalama , jasusi namba moja duniani kwa upande wa wanawake
Za Kitaa/Street Talks
Huyu ndiye Bertrand Bisimwa anayeendesha maisha yake kwa kuanzisha makundi ya waasi nchini Kongo
Za Kitaa/Street Talks
Aa
LiwalonaliweLiwalonaliwe
Aa
Search
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Focused Affairs
    • Dating
    • Career
    • Kijiweni
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Liwalonaliwe > Kijiweni > DR Congo yataka maelezo kuhusu vitisho vya jenerali Muhoozi wa Uganda
Kijiweni

DR Congo yataka maelezo kuhusu vitisho vya jenerali Muhoozi wa Uganda

Baraka Bitariho
Last updated: 2026/11/26 at 3:24 PM
Baraka Bitariho
Share
SHARE
0
SHARES
ShareTweet

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) imemwita mwanadiplomasia mkuu wa Uganda mjini Kinshasa kufuatia machapisho ya mitandao ya kijamii ya mkuu wa jeshi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mwana wa rais wa nchi hiyo.

Katika mfululizo wa machapisho kwenye mtandao wa X, Jenerali Kainerugaba alionekana kuunga mkono uwezekano wa waasi kuiteka Walikale, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa DR Congo. Hata hivyo, alisisitiza kuwa uwepo wa jeshi la Uganda nchini humo unalenga masuala ya usalama pekee.

Wizara ya Mambo ya Nje ya DR Congo ilimwita balozi wa Uganda kueleza matamshi hayo, ikiyataja kuwa “ya hatari sana” na yanayoweza kuathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Serikali ya Uganda haikuwa imetoa majibu yoyote kufikia sasa.

Mvutano huu wa kidiplomasia umeibuka licha ya ushirikiano wa karibu wa kijeshi kati ya nchi hizo jirani.

Tangu mwaka 2021, majeshi ya Uganda na DR Congo yamekuwa yakifanya operesheni za pamoja dhidi ya kundi la Allied Democratic Forces (ADF), lenye uhusiano na kundi la Islamic State, mashariki mwa DR Congo.

Uganda pia imekuwa ikihusika katika juhudi za upatanishi kati ya serikali ya Congo na kundi lenye silaha linaloongozwa na aliyekuwa mbabe wa vita, Thomas Lubanga, katika jimbo la Ituri.

Katika machapisho yake, Jenerali Kainerugaba aliishutumu Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), kundi lenye silaha linalofanya shughuli zake mashariki mwa DR Congo, kwa kuwalenga watu wa jamii ya Bahima.

Wabahema ni jamii ya wafugaji wa jadi inayopatikana zaidi katika jimbo la Ituri kaskazini mashariki mwa DR Congo. Jamii hiyo ina uhusiano wa kihistoria na kitamaduni na Wabahima wa Uganda.

Jenerali huyo pia alitoa vitisho vya kuungwa mkono kwa utekaji wa Walikale na waasi, huku akitetea uwepo wa jeshi la Uganda nchini DR Congo.

Walikale ni eneo lenye utajiri mkubwa wa madini, likiwemo baadhi ya machimbo makubwa ya bati na dhahabu nchini humo.

Akaunti ya X ya Jenerali Kainerugaba, iliyokuwa na karibu wafuasi milioni 1.4, baadaye haikuweza kupatikana.

Haijulikani iwapo aliifunga mwenyewe kama alivyowahi kufanya hapo awali au kama jukwaa hilo liliisimamisha.

Katika wiki hiyo hiyo, alitangaza:

“Machapisho yangu kwenye X nchini Uganda ni maagizo ambayo lazima yatekelezwe.”

Sign Up For Daily Newsletter

Be keep up! Get the latest breaking news delivered straight to your inbox.
[mc4wp_form]
By signing up, you agree to our Terms of Use and acknowledge the data practices in our Privacy Policy. You may unsubscribe at any time.
Baraka Bitariho November 26, 2026
Share this Article
Facebook Twitter Pinterest Whatsapp Whatsapp LinkedIn Copy Link Print
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

LiwalonaliweLiwalonaliwe
Follow US

© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

[mc4wp_form]
Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Register Lost your password?