*Avila Chaula* ni Binti ambaye anafanya vizuri kwenye sekta ya urembo nchini Tanzania hasa katika ususi na make up
Avila Chaula ni Mkurugenzi wa Allie Stylish saloon mbayo ni Saloon bora ya wanawake inayofanya vizuri nchini Tanzania.
Kupitia kampuni yake ya Stylish saloon ameweza kuteka soko la urembo hapa nchini kutokana na kutoa huduma bora na zenye ubunifu mkubwa zinazowavutia wateja wa urembo hapa nchini .
Avila Chaula kupitia Allie Stylish anamiliki saloon mbili za kisasa ambazo zinapatikana manzense ,Dar es salaam pamoja na Zanzibar kisauni.
Avila Chaula amekuwa ni mbobezi kwenye fani ya ususi Kwa kuwasuka wanawake mitindo mbalimbali ya nywele ambapo hali hiyo imesabisha ajizolee umaarufu nchini Tanzania…
Anasema alianza fani ya ususi akiwa darasa la nne ambapo mwaka 2018 alianza rasmi ya ususi Kwa kusuka watu nyumbani kwake na kuwafuata watu nyumbani kwao mpaka kufikia hatua ya kufungua ofisini.
Licha ya hivyo amekuwa anatoa elimu ya ususi na make up kwa watu mbalimbali nchini Tanzania .
Katika kuelezea safari yake mpaka kufika hatua hii anasema alipomaliza kidato Cha sita alijiunga na chuo Cha maji lakini hakufanikiwa kumaliza kutokana na kupata changamoto ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake, Alipata udhamini wa kwenda kusomea urembo katika chuo kikuu huria na baadae alienda kupata elimu katika chuo Cha veta.
Kutokana kuwa na kipaji na pamoja na elimu ya urembo hali hii imemsaidia afanye kazi ya urembo kwa ufanisi mkubwa sana .
Ameweza kupata ya tuzo ya Ususi bora nchini Tanzania inayojulikana kama Business Award .
Ameweza kuandaa tukio kubwa linalojulikana kama stitching master class yenye lengo la kutoa elimu na ujuzi kwa wasusi mbalimbali nchini Tanzania ili waweze kuongeza ujuzi ,maarifa katika kazi yao ya ususi ambapo tukio hilo kubwa lilidhaminiwa na kampuni ya prima Afro hair.
kwa huduma za urembo unaweza kuwasiliana nae kupitia namba ya simu
0678182070
Pia kwa whatsapp 0678182070
