
Huyu ndiye Bertrand Bisimwa anayeendesha maisha yake kwa kuanzisha makundi ya waasi nchini Kongo
**Anaitwa Bertrand Bisimwa ni mwanasiasa mashuhuri wa Kongo, mtaalamu wa sheria na kiongozi wa waasi, ambaye amekuwa Rais wa (M23) kwa muda mrefu sana.
**Baada ya Joseph kabila kuungana M-23 na kuanzisha Front for the Refoundation of the Nation (FRN) amechaguliwa Kuwa makamu wa rais wa kundi hilo.
**Alizaliwa tarehe 8 Septemba 1972 huko Bukavu na ametumia miongo kadhaa akiwa amejikita katika kufanya uasi na migogoro ya kutumia silaha inayoikabili eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
**Bisimwa alianza safari yake ya uasi mwaka 1996 akiwa na kundi la Alliance des Forces Démocratiques pour la Libération du Congo (AFDL), ambalo lilifanikiwa kumuondoa madarakani Mobutu Sese Seko.
**Mnamo mwaka 1998 alienda kufanya uasi mwingine Kwa kujiunga na kundi la Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD) ili kupambana na serikali za Laurent-Désiré Kabila na Joseph Kabila.
**Baadaye alikuwa msemaji wa kundi la Laurent Nkunda, National Congress for the Defense of the People (CNDP).kundi hili kilifanya maafa makubwa Kongo ambapo kwasasa Nkunda anaishi Rwanda .
**Mwaka 2013 Bisimwa alijiunga kwenye uasi mwingine alichukua nafasi ya Jean-Marie Runiga kama kiongozi wa tawi la kisiasa la M23,Bisimwa alisimamia operesheni kubwa za kundi hilo katika eneo la Kivu Kaskazini,
***Mwaka 2013 baada ya jeshi la Tanzania kutoa kipigo cha mbwa huko Kongo
Bisimwa alikimbilia nchini Uganda.
**Hivi karibuni akiwa
ni Mmoja wa viongozi wa AFC na M23 alijiunga na Mungu jipa la kisiasa na kijeshi linaloitwa Front for the Refoundation of the Nation (FRN) ambalo lipo chini ya Joseph kabila kupambana na serikali ya Kongo .
