
**Waziri mkuu wa Rwanda ambaye unaweza kumwita baba kipenyo.
**Anaitwa Justin Nsengiyumva ambaye kwasasa ni waziri mkuu wa Rwanda
**Inadaiwa hapo awali alipandikizwa ndani ya Muungano wa upinzani wa Rwanda Yan (RNC) huko Ulaya.
**Huyu ni jasusi wa muda mrefu aliyefanikiwa kupenya ndani kabisa ya upinzani wa Rwanda huko Ulaya
***Mwaka 2008 Pitia njia za kikachero alisafiri kwenda Uingereza kupitia Uganda, akaomba hifadhi ya ukimbizi ambapo alifanikiwa kupata hadhi ya mkimbizi ambapo alikaa Uingereza kwa zaidi ya miaka 15.
**Baada kuishi na kufanya kazi Ulaya alipata uraia wa Uingereza na kujipatia umaarufu ndani ya chama cha Rwanda National Congress
akitumia nafasi hiyo hiyo kupeleleza upinzani .
**Alipata PhD Katika uchumi kutoka chuo Kikuu Cha Leicester nchini Uingereza.
**Alifanya kazi Katika serikali ya Uingereza kama mchumi mwandamizi na mshauri wa masuala ya kiuchumi katika taasisi za serikali ya Uingereza.
**Justin Nsengiyumva alijifanya mpinzani na alikuwa na sifa zote kuonekana ni mpinzani wa Rwanda, alionekana kama mkimbizi wa kawaida mwenye asili ya kabila la Kihutu kutoka eneo la kaskazini la Musanze (zamani Ruhengeri), jambo lililomsaidia kukwepa kutiliwa mashaka na wenzanke kutoka upande wa upinzani
Ingawa ilijulikana sana kuwa hapo awali aliwahi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu ya Rwanda na kushikilia nyadhifa nyingine muhimu, na kwamba akiwa Uingereza aliendelea kupokea mapato ya kodi kutoka kwa mali zake nchini Rwanda, ukweli huo ulipuuzwa kutokana na asili yake ya kikabila na ya kikanda.
**Akiwa ndani ya chama cha upinzani (RNC) Nsengiyumva alichukuliwa kama mtu muhimu akipata taarifa za siri za kiutendaji za Chama hicho Cha upinzani.
**Justin Nsengiyumva
alifanikiwa kufanya kazi aliyotumwa ambapo alisabaratisha RNC na kudhoofisha sana muungano wa P5,
**Mwaka 2025 Nsengiyumva aliitwa na kurejea na kurejea Rwanda Mnamo tarehe 25 Februari 2025, aliteuliwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Rwanda, uteuzi huo uliowashangaza sana wenzake katoka upinzani.
**Tarehe 23 Julai 2025, aliteuliwa na rais kagame Kuwa Waziri Mkuu wa Rwanda
