
**Katika vita ya ujasusi hapa duniani nchi inaweza kumtaka jasusi wao ajitangaze hadharani kwamba aliweza kuingia nchi adui na kukusanya taarifa bila wao kujua .
**Mfano Marekani inaweza kumtaka jasusi atangaze hadharani kwamba aliweza kuingia Iran na kukusanya taarifa muhimu bila wao kujua.
**Mfano Urusi inaweza kumtaka jasusi wao atangaze hadharani kwamba aliweza kuingia Marekani na kukusanya taarifa muhimu bila wao kujua.
**Kitendo cha nchi kumtaka jasusi wao ajitangaze hadharani ili kuonesha uwezo na kutengeneza hofu kwa adui kinaitwa Ufichuzi wa Kimkakati
#Strategic#Disclosure / Strategic Declassification
**Katika tasnia ya usalama na ujasusi, mbinu hii inavunja ule mwiko wa kawaida wa “usiri wa maisha yote” kwa malengo maalum ya kisiasa na kijeshi,kijasusi
***Kuweka hadharani taarifa za siri au mafanikio ya kijasusi kwa makusudi kamili ni Kutuma ujumbe wa onyo kwa adui ajue kuwa “tupo ndani ya mifumo yenu na tunajua kila kitu,” hali inayomfanya adui kujawa na wasiwasi na kuanza kujishuku ndani.
**Adui anapoona kuwa siri zake zote ziko wazi, anaweza kusitisha mipango yake ya vita au uhujumu kwa hofu ya kushindwa au kuaibika.,
*Kitendo hiki kinaangukia pia kwenye vita vya kisaikolojia. Lengo kuu si kuua kwa risasi, bali ni kuuharibu kisaikolojia upande wa adui na kuwavunja moyo majasusi wao na kuwafanya waamini kuwa taasisi zao za usalama zimefeli vibaya sana
