Na Sam Ruhuza
Sasa inatosha!!
Chama halali cha siasa, viongozi na wanachama wake wanakutana na kuamua kuwaombea wananchi wenzao waliopotea kwa kutekwa na wanaoitwa ‘watu wasiojulikana!’, wengine wanaamua kwenda nyumbani kwa aliyetekwa kuifariji familia, Police anatokea na kuwazuia na kuwakamata!!!
Hii kwetu wananchi inatupa tafsiri gani kati ya Police na ‘watu wasiojulikana’?
Kuna matukio mengine yanatokea hadi mtu unajiuliza, hii ni kweli??!!
Hao Chadema na Police kuna shida gani?! Mbona ukamataji na ubabe mwingi!, Kulikoni?!
Kumbukeni hao ni Watanzania na wana Haki!

Tunahubiri sana Amani, tunasahau HAKI ndio mzizi. Haki ikiwapo, amani ipo tu yenyewe, ila unapozuia Haki, lazima anayezuiwa ataidai tu na wewe utajitahidi kumzuia na hapo Amani inajitenga mbali kabisa!
Hata Mtoto mchanga anajua haki yake ya nyonyo, unapomzuia, atalia tu na utakosa amani kwa kelele zake, sembesu watu wazima??!!
Pls, Pls, Pls, Police kaeni mbali na mambo ya kisiasa, huko sio kwenu, mnafanya vizuri kwenye ulinzi wa mengine, lakini huku kwenye siasa wanawaingiza kuwachafua ili kutengeneza hasira na wananchi!

Watawala acheni Police wafanye kazi zao za msingi, haya ya siasa pambana mwenyewe kwenye majukwaa, tunaipenda Amani, toa Haki!
Tanzania ni yetu sote! 


