By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
LiwalonaliweLiwalonaliwe
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Kijiweni
  • Dating
  • Career
Search
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Reading: #Huyu ndiye Jeannette Kagame mke wa rais #Paul kagame
Share
Sign In
Notification Show More
Latest News
Historia ya rais wa Burundi mhe: Évariste Ndayishimiye
Uncategorized
Pigo kwa Benjamini Netanyahu: Eisenkot akabidhiwa jukumu la kuunda serikali mpya ya Israel
Uncategorized
Mwanaharakati wa demokrasia Joshua Wong ahukumiwa kifungo cha miaka 10 zaidi jela
Uncategorized
Kutana na mwanajeshi wa Rwanda aliyeuawa kwa kukatwa kichwa nchini Uganda
Uncategorized
Kutana na jasusi kutoka kenya aliyetekwa na kupotea
Uncategorized
Aa
LiwalonaliweLiwalonaliwe
Aa
Search
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Focused Affairs
    • Dating
    • Career
    • Kijiweni
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Liwalonaliwe > Uncategorized > #Huyu ndiye Jeannette Kagame mke wa rais #Paul kagame
Uncategorized

#Huyu ndiye Jeannette Kagame mke wa rais #Paul kagame

Baraka Bitariho
Last updated: 2026/11/07 at 6:43 PM
Baraka Bitariho
Share
SHARE
May be an image of text

#Huyu ndiye Jeannette Kagame mke wa rais #Paul kagame#Alizaliwa nchini #Burundi

**Anaitwa Bi Jeannette Nyiramongi Kagame ambaye ni mke wa rais Kagame.

**Bi Jeanette Nyiramongi Kagame alizaliwa ukimbizini katika nchini Burundi tarehe 10 Agosti, 1962

**Wazazi wake walikuwa wakimbizi nchini Burundi kufuatia machafuko ya kikabila yaliyoikumba Rwanda.

*”Alizaliwa kipindi kifupi baada ya Rwanda kupata uhuru wake kutoka kwa ukoloni wa Kibelgiji.

**Elimu yake ya msingi na sekondari aliipata nchini Burundi, ambako alisomea katika shule ya sekondari ya St Albert

,**Jeanette Nyiramongi Kagame baadaye aliendelea na masomo yake Nairobi, Kenya ambako wazazi wake walikuwa wanaishi kama wakimbizi.

**Akiwa mjini Nairobi nchini Kenya alipokuwa anaishi na wazazi wake, Bi Jeanette Nyiramongi alikutana na rais Paul Kagame wakachumbiana na baadaye kuoana na ndipo alipoanza kuitwa Jeannette Kagame.

**Harusi yao ya kufana ilifanyika nchini Uganda ambapo kipindi hicho mme wake Bw Paul Kagame alikuwa akiishi kama mkimbizi nchini Uganda, lakini wakati huo akiwa mwanajeshi katika jeshi la Uganda.

** Bi Jeanette Kagame alikabiliwa na jukumu la kuwa mke wa mwanajeshi Paul Kagame ambaye baadaye miaka ya 90 alijiunga na mapambano ya vita vya waasi wa RPF vilivyolenga kulikomboa taifa la Rwanda na kuwarejesha nyumbani Wanyarwanda waliokuwa ukimbizini, vita ambavyo aliviongoza Mme wake Paul Kagame, baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa kundi la RPF Fred Rwigema.

**Mwaka 1994, majeshi ya RPF yalipata ushindi na Bi Jeanette Kagame alirudi Rwanda pamoja na familia yake, kushirikiana na mme kulijenga taifa lililokuwa limesabaratishwa vibaya kwa vita na mauaji ya kimbari

**Bi Jeanette Kagame na mmewe Paul Kagame wamejaliwa watoto wanne wa kiume watatu na wa kike mmoja, wa kwanza akiwa ni Yvan Cyomoro Kagame, wa pili Ange Ingabire Kagame, wa tatu Ian Kagame na kitinda mimba akiitwa Brian Kagame.

**Bi Jeanette Kagame baada ya kurejea nchini Rwanda kutoka ukimbizini alijitokeza kama mtu aliyejitolea kuinua maisha ya Wanyarwanda wenye matatizo mbalimbali ya kijamii, hususan maisha ya wajane,l

*Tarehe 28 Februari 1996 aliunda Shirika la (Unity Club) ambalo lengo lake limekuwa ni kuwaleta pamoja mawaziri na wabunge wanawake na wake wa mawaziri kwa lengo la kuboresha umoja na amani huku wakichangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kufuatia mauaji ya kimbari na sasa shirika hilo lina wajumbe zaidi ya 270 likiwajumuisha viongozi wanaume.

**Kuanzia tarehe 24 Machi, 2000, Jeannette Kagame alitambulilika rasmi kama Mke wa rais, baada ya mumewe Paul Kagame kuwa rais nne wa Rwanda.

**Mwaka 2002 alianzisha Wakfu wa Imbuto Foundation, ambao umekuwa na mchango mkubwa katika kutoa usaidizi wa elimu kwa watoto hususan wa kike wanaotoka katika familia masikini.

Sign Up For Daily Newsletter

Be keep up! Get the latest breaking news delivered straight to your inbox.
[mc4wp_form]
By signing up, you agree to our Terms of Use and acknowledge the data practices in our Privacy Policy. You may unsubscribe at any time.
Baraka Bitariho November 7, 2026
Share this Article
Facebook Twitter Copy Link Print
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

LiwalonaliweLiwalonaliwe
Follow US

© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

[mc4wp_form]
Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Register Lost your password?