By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
LiwalonaliweLiwalonaliwe
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Kijiweni
  • Dating
  • Career
Search
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Reading: Inatosha!!
Share
Sign In
Notification Show More
Latest News
Kipi Bora: Mira ama taratibu za kidini
Kijiweni
Kuporwa Passport Tanzania
Uvumi
Ninawaza kwa sauti!!
Kijiweni
DC Ngara Katika Hili Umechemka, Kama ni Kweli Waombe Radhi Vijana
Uvumi
Ukimya ni Uoga ama ni Usalama?
Uvumi
Aa
LiwalonaliweLiwalonaliwe
Aa
Search
  • Uvumi
  • Za Kitaa/Street Talks
  • Focused Affairs
    • Dating
    • Career
    • Kijiweni
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Liwalonaliwe > Za Kitaa/Street Talks > Inatosha!!
Za Kitaa/Street Talks

Inatosha!!

Mzee
Last updated: 2025/09/07 at 10:24 PM
Mzee
Share
Tanzania ni nchi inayopitia katika wakati mgumu ambao yata polisi anakili kutojua kikundi kinachoitwa watu wasiojulikana. Kazi ya polisi ni kulinda ila mlinzi anapokiri kutojua aliyeiba, sasa haifahamiki kama anashindwa kutimiza kazi yake ama kama anatii mashariti kutoka kwa anayemlipa mshahara. Ila anayemlipa mshahara ni mwananchi na sio mkata cheki kila mwezi. Watanzania wengi wanasubiria kujua hao wasiojulikana watajulikana lini kwani mkono unaotumika kwa baadhi ya watanzania unakua mzito sana kuliko wengine ama hata kuangalia pembeni ili kile kinachofanywa na wale wanaoangushiwa nyundo baadala ya kuelekezwa, waendelee kwa uhuru. Pengine utanzania wa wale wanaoachiwa kuendelea na yao ndio wenye haki kwani utanzania wao ni mzito zaidi. Wale ambao utanzania wao ni kwa jina tuu kinachowafaa ni nyundo yenye meno kwani wanachokigombania hawana haki nacho.
SHARE

Na Sam Ruhuza

Sasa inatosha!!

Chama halali cha siasa, viongozi na wanachama wake wanakutana na kuamua kuwaombea wananchi wenzao waliopotea kwa kutekwa na wanaoitwa ‘watu wasiojulikana!’, wengine wanaamua kwenda nyumbani kwa aliyetekwa kuifariji familia, Police anatokea na kuwazuia na kuwakamata!!! 

Hii kwetu wananchi inatupa tafsiri gani kati ya Police na ‘watu wasiojulikana’? 

Kuna matukio mengine yanatokea hadi mtu unajiuliza, hii ni kweli??!! 

Hao Chadema na Police kuna shida gani?! Mbona ukamataji na ubabe mwingi!,  Kulikoni?! 

Kumbukeni hao ni Watanzania na wana Haki! 

Haki ni kwa Watanzania. Kura ziliibiwa na wasiojulikana. Si vituo vya kura vinalindwaga ama mlinzi aliangalia pembeni wasiojulikana wakafanya yao? Haya ni maswali magumu ila yanaumuhimu na si kupuuzwa. Haki ya Mtanzania ilindwe na kama kuna watanzania wasiokuwa na haki, basi na hilo lijukane.

Tunahubiri sana Amani, tunasahau HAKI ndio mzizi. Haki ikiwapo, amani ipo tu yenyewe, ila unapozuia Haki, lazima anayezuiwa ataidai tu na wewe utajitahidi kumzuia na hapo Amani inajitenga mbali kabisa! 

Hata Mtoto mchanga anajua haki yake ya nyonyo, unapomzuia, atalia tu na utakosa amani kwa kelele zake, sembesu watu wazima??!! 

Pls, Pls, Pls, Police kaeni mbali na mambo ya kisiasa, huko sio kwenu, mnafanya vizuri kwenye ulinzi wa mengine, lakini huku kwenye siasa wanawaingiza kuwachafua ili kutengeneza hasira na wananchi! 

Waliopewa jukumu la kulinda raia na mali zao wakikili ufukuaji wa kaburi na mwili kuibiwa umefanywa na kundi la wale wasiojulikana kwani ulinzi ni kwa wananchi na mali zake. Haijulikani kama aliyefariki alikua si mtanzania tena ama kama utanzania unaisha pale pumzi inapoachana na mwili.

Watawala acheni Police wafanye kazi zao za msingi, haya ya siasa pambana mwenyewe kwenye majukwaa, tunaipenda Amani, toa Haki! 

Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿🤝💪

Sign Up For Daily Newsletter

Be keep up! Get the latest breaking news delivered straight to your inbox.
[mc4wp_form]
By signing up, you agree to our Terms of Use and acknowledge the data practices in our Privacy Policy. You may unsubscribe at any time.
Mzee September 7, 2025
Share this Article
Facebook Twitter Copy Link Print
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LiwalonaliweLiwalonaliwe
Follow US

© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

[mc4wp_form]
Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Register Lost your password?