Habari za leo wapendwa wasomaji. Leo ningependa kutoa ripoti kuhusu hali ya kuhuzunisha ya matokeo ya kozi ya uwakili kutoka shule ya Sheria Tanzania. Kati ya wanafunzi 821 waliofanya mtihani, ni wanafunzi 23 pekee waliofaulu, sawa na asilimia 2.8%, huku asilimia 97.2 wakidaiwa kufeli. Hali hii inajiri baada ya malalamiko mengi kutolewa na wadau wa elimu kufuatia matokeo ya mwaka jana, ambapo wanafunzi 26 pekee kati ya 633 waliofanya mtihani walifaulu.
Kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri wa Sheria na Katiba, @damasndumbaro_official chini ya uongozi wa @harrisonmwakyembe, iliwasilisha taarifa yake, ambapo ilidai kuwa tatizo ni uwezo mdogo wa wanafunzi unaotokana na vyuo walivyosoma. Hata hivyo, matokeo ya mwaka huu yanaibua maswali zaidi kuhusu hali hiyo.
Kuna malalamiko kuwa Kamati ya Mwakyembe ilifanya uchunguzi wa kina, lakini haikufanya ‘rundom sampling’ ambayo ingewezesha kupata picha halisi ya tatizo. Kwa kuwa walimu walikuwa wengi kuliko wanafunzi waliohojiwa, inawezekana kuwa kuna tatizo kubwa zaidi ambalo halitajwi. Huwezi kufundisha darasa la watu 100 wakafaulu wawili tu, halafu ukajitetea eti ni uwezo mdogo wa wanafunzi. Uchunguzi zaidi unahitajika ili kubaini chanzo cha tatizo hili la kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika kozi hii muhimu. Tutawaarifu kuhusu maendeleo zaidi ya suala hili. Asanteni sana.
Imetumwa na: AMK